Msichana mwenye macho ya kijani ailiyekuwa ishara ya madhira ya Afghanstan yanayoendelea, amewasili nchini Italia na amepewa hifadhi na serikali ya nchini hiyo.
Msichana huyo alipata umaarufu wa kimataifa wakati chombo maarufu cha habari cha kimataifa - National Geographic kilipochapisha picha yake kwenye jarida lake mwaka huu . Msichana huyo kwa jina Sherbat Gul alikuwa na umri wa miaka 9 wakati huo.
Ofisi ya Wazriri mkuu wa Italia Mario Draghi Alhamisi ilithibitisha kuwa msichana huyo amewasili katika mji mkuu Roma.
Mpigapicha wa msichana huyo aliyeitwa ua la sherbet alichapisha picha yake mwaka 2006, aliyopigwa akiwa mtoto na Steve McCurry, mpigapicha wa jarida la -National Geographic , na kumpatia umaarufu wa kiataifa na kumfanya kuwa mmoja wa wakimbizi maarufu zaidi wa Afghanistan.