Msanii wa Bongo, Jacqueline Fitzpatrick ‘Jack Patrick’.
BAADA ya kufanikiwa kuyachomoka maisha ya jela aliyosota nayo kwa miaka takriban 7, msanii wa Bongo, Jacqueline Fitzpatrick ‘Jack Patrick’ amezidi kuzua sintofahamu.
Inaelezwa kwenye mitandao mingi ya kijamii kwamba atabanwa awataje washirika wake aliokuwa akidili nao biashara haramu ya madawa ya kulevya.
Hofu na matarajio ya Jack Patrick kufanya hivyo baada ya kutoka jela imekuwepo tangu aliponaswa Desemba 19, mwaka 2013, akiwa na madawa aina ya Heroin kilo 1.1, katika Kisiwa cha Macau nchini China ambako baadaye alifungwa jela.
Maswali na mawazo ya wengi ni kwamba; Je, sheria inamlazimisha kuwataja aliokuwa akishirikiana nao na kwamba huenda akala kibano kutoka kwenye mikono ya dola?
Ikiwa atawataja waliomtuma kusafirisha madawa hayo; atakaowataja watakamatwa na kupelekwa mahakamani?
Usalama wa Jack Patrick utakuwaje endapo ataamua kuutaja mtandao wa madawa ya kulevya ambao alikuwa akishirikiana nao enzi hiyo?
Maisha ya Jack baada ya kutoka gerezani yatakuwaje mbele ya jamii ambayo zamani ilikuwa inamuona ni kioo cha jamii?
Kabla ya kuleta majibu ya maswali haya; kila mmoja afunguke ufahamu wake nini anachoelewa; majibu konki yatakuja baadaye.