Jambazi aliyesakwa kwa miaka 52 akamatwa Marekani




Jambazi sugu wa wizi wa benki nchini Marekani ametambuliwa baada ya msako wa miaka 52, maafisa wa sheria wametangaza.

Ted Conrad alikua akihudumu kama kama keshia katika benki Society National mjini Clevland, Ohio alipomuibia muajiri wake mnamo 1969.

Alitoweka na jumla ya dola dola 215,000, zenye thamani ya dola milioni 1.7 kwa sasa.

Wachunguzi kutoka Huduma ya Wanajeshi wa Marekani walisema baadaye aliishi maisha ya utulivu na ya kujistahi.

Conrad, ambaye alifariki mwezi Mei kutokana na saratani , alikuwa na miaka 20 tu wakati alipofanya wizi huo. Aliripotiwa kutumia utepetevu wawalinzi wa benki hiyo, kutoka na hela zilizokuwa zimefichwa kwenye mfuko wa plastiki wakati walipofunga kazi Ijumaa jioni.

Wanyakazi wengine wa benki hiyo waligundua hela zimetoweka siku mbili baadaye, Conrad alikuwa ametoweka.

Aliibua msako ambao ungedumu kwa zaidi ya nusu karne na kesi hiyo iliendelea kuonyeshwa kwenye vipindi vya televisheni kama vile America's Most Wanted and Unsolved Mysteries.

Kulingana na Huduma ya wanajeshi, Conrad alidaiwa kuwaambia marafiki zake juu ya mipango yake ya kuiba benki na kujigamba jinsi ingekuwa rahisi kufanya hivyo.

Inasemekana kuwa alivutiwa na filamu ya Steve McQueen ya mwaka wa 1968, The Thomas Crown Affair, na kuitazama zaidi ya mara kumi na mbili wakati wa maandalizi yake ya wizi huo.

Wanajeshi wanasema baada ya kutoweka Conrad alibadilisha jina lake kuwa na kutorokea Washington D.C na Los Angeles, kabla ya kuishiviungani mwa Boston karibu kilo mita 1000 kutoka eneo la uhalifu huo.

Wachunguzi wanasema baadaye aliishi maisha ya utulivu na ya kujistahi na gazeti la New York Times liliripoti kwamba alikuwa ametumia miaka 40 iliyopita akifanya kazi kama mtaalamu wa gofu na kuwamuuzaji wa magari yaliyotumika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad