#GetToKnow Jana Jumatano mitandao yote duniani ililipuka baada ya jina la Jay-Z kuonekana kwenye mtandao wa Instagram, akiripotiwa kujiunga na mtandao huo kwa mara ya kwanza licha ya ripoti kuonesha aliwahi kufanya hivyo mwaka 2015. Sasa Jay-Z ameendelea kuthibitisha kuwa sio mtu wa mitandao ya Kijamii, kwani ameamua kuiondoa akaunti hiyo asubuhi hii ikiwa na followers zaidi ya milioni 2 na kitiki cha blue.
Jay-Z ni kama alikuwa na lengo la kuitangaza tu filamu yake ya "The Harder They Fall" ambayo amehusika kama mtayarishaji. Filamu hiyo ilioneshwa Jana kwa mara ya kwanza kupitia Jukwaa la Netflix.