Neno "KUBEMENDA MTOTO" limekuwa likitumika kutafsiri,KUDHOOFIKA au KUZOROTA kwa afya ya Mtoto, au Mtoto KUDUMAA na Kutokukua Inavyotakiwa
IMANI ILIYOJENGEKA NI KUWA
1. wazazi wakishiriki Tendo la ndoa baada ya mama kujifungua hata kama 40 Imepita WANAWEZA KUBEMENDA MTOTO,kwa kuwa mbegu za mwanaume zinaenda kwenye maziwa ya mama zinadhoofisha afya ya mtoto,
2. Mama akipata MIMBA, huku akiwa na mtoto mchanga wa Miezi kadhaa ANABEMENDA MTOTO
3. Mtoto Mchanga Akinyonya maziwa ya Mama ambae ni mjamzito ATABEMENDWA
4. Mwanandoa Akitoka nje ya NDOA akazini huko,akirudi kushiriki tendo la ndoa na mwenzie wanabemenda mtoto.
5. Ukitoka kushiriki tendo la ndoa halafu ukamgusa mtoto ANABEMENDWA🤔🙆🏿♂️
Sababu HIZO ZOTE SIO KWELI-
Hakuna uhusiano wa kisayansi na sababu ambazo jamii inazitaja
Vyanzo vikubwa vya mtoto Kutokukua Inavyotakiwa ni
1. Mtoto kutokupata maziwa ya kutosha (mama hanyonyeshi,au hana maziwa ya kutosha au mtoto hanyonyi)
2. Magonjwa kama Ukimwi,magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo,pneumonia...
3. Mtoto kukosa lishe inayofaa,yaan utapiamlo pia huwa unadhoofisha mtoto na kuleta shida kwenye Ukuaji.
Kitaalamu Mke na Mume wanaruhusiwa kufanya tendo la ndoa mara tu baada ya SIKU 42 KUPITA Tangu kujifungua.
Muhimu ni Haya
1. Mama Anyonyeshe Mtoto wake ipasavyo mara kwa mara(asipozingatia italeta shida kwenye ukuaji wa mtoto)
2. Mtoto anyonye miezi 6 pasipo kumpa kitu kingine chochote,akifika Miezi 6 hakikisha unampa lishe Bora(lishe yenye makundi yote ya vyakula) ili asipate utapiamlo
3. Kutoka Nje ya ndoa yako ni Hatari maana unaweza pata magonjwa ya kuambukizwa kama Maambukizi ya VVU (iwe baba,iwe Mama,ni hatari,mwisho wa siku unaweza kumwambukiza mtoto na kuathiri ukuaji wake)
Hii ni kwa mujibu wa mtaalamu wa Afya kutoka kituo cha Mbezi Health Clinic Anusiata Pius.