Mbunge wa Ukonga Jerry Silaa amemuomba radhi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai.
“Nimepokea kwa moyo mkunjufu azimio la Bunge na maelekezo ya Mh. Spika ya kikao cha August 31 2021, kidhati namuomba radhi Mh. Spika, Bunge na Wabunge” amesema Mbunge huyu Ukonga.
Katika kikao hicho Bunge liliwapa adhabu Wabunge @JerrySilaa na Josephat Gwajima kwa utovu wa nidhamu ambapo hawatotakiwa kuhudhuria vikao vya Bunge mpaka January 2022.