Jopo la uchunguzi, lililoundwa na mamlaka nchini Nigeriakuchunguza tukio la waandamanaji kupigwa risasimjiniLagos mnamo Oktoba2020, limewasilisha ripoti juu ya kile kilichokea usiku huo.
Toleo lililovuja la ripoti hiyo, iliyokabidhiwa kwa gavana wa jimbo hilo leo, inadai kuwa wanajeshi wa Nigeria waliwapiga risasi kimakusudi waandamanaji waliokuwa wakipinga ukatili wa polisi kwenye barabara ya Lekki Tollgate, kisha wakajaribu kuificha.
Waandamanaji hao walikuwa wakiendesha kampeni dhidi ya ukatili wa polisi.
Pia ilibaini kuwa baada ya jeshi hilo kurudi nyuma, askari polisi waliendelea na vurugu na kujaribu kufanya usafi katika eneo la tukio na kuweka miili kwenye lori na kutoa risasi.
Baadhi ya matokeo yanalingana na ripoti za awali za Amnesty International, pamoja na vyombo vya habari vya ndani na kimataifa.
Gavana wa Jimbo la Lagos Babajide Sanwo-Olu, ambaye alianzisha jopo hilo, ameahidi "kutilia maanani" matokeo yake.