Jinsi Papara za Kibu Denis Zilivyoinyima SIMBA Magoli Tisa Kilaini, Matola Ashindwa Kujizuia

 


KAMA ingekuwa ni utulivu wa mshambuliaji wa Simba Kibu Dennis akiwa ndani ya 18 basi kwa sasa angekuwa yupo kwenye orodha ya wakali wa kucheka na nyavu kutona na nafasi ambazo amekuwa akizipata na kushindwa kuzitumia.

Rekodi zinaonyesha kuwa ni jumla ya nafasi tisa za wazi aliweza kutengeneza huku katika nafasi hizo akifunga bao moja pekee likiwa ni la kwanza kwake baada ya kujiunga na Simba akitokea kikosi cha Mbeya City.


Mchezo wake wa kwanza ndani ya Simba ilikuwa mbele ya Polisi Tanzania, Oktoba 27 Uwanja wa Mkapa na alitumia dakika 45 alikosa nafasi moja ya wazi.Mchezo wa pili ilikuwa mbele ya Coastal Union, Oktoba 31 wakati ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 0-0 Coastal Union hapa alikosa nafasi mbili za wazi na alitumia dakika 90.


Mchezo wake wa tatu ilikuwa ni Novemba 3 mbele ya Namungo ubao uliposoma Simba 1-0Namungo alikosa nafasi mbili pia za wazi na alitumia dakika 90.


Mchezo wake wa nne ndani ya Simba rasta huyo alitumia dakika 90 Novemba 19 mbele ya Ruvu Shooting, Uwanja wa CCM Kirumba alikosa nafasi tatu ikiwa ni pamoja na ile akiwa na kipa Mohamed Makaka dakika ya 90 hivyo angetulia angeweza kufunga mabao manne kama tu angekuwa na utulivu.


Mpaka sasa ametumia dakika 315 kwenye ligi na kwa mujibu wa Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola alisema kuwa kikubwa ambacho kinaipa tabu safu ya ushambuliaji ni presha jambo ambalo linafanyiwa kazi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad