Mahabusu Shadrack Leparan (29), Enoc Ndege (28) na Patrick Mausa (32) wametoroka kwenye kituo cha Polisi walikokua wakishikiliwa usiku wa kuamkia Jumamosi huko Narok nchini Kenya baada ya kufanikiwa kutoboa shimo kwenye ukuta wa seli ambayo walikuwa wamewekwa.
Polisi watatu waliokuwa zamu usiku huo wamekamatwa kutokana na uzembe waliofanya mpaka Mahabusu hao watatu kutoroka siku mbili kabla ya tarehe yao ya kufikishwa Mahakamani, tukio hili limetokea siku mbili tu baada ya kukamatwa kwa Washukiwa wa Ugaidi ambao walitoroka kwenye jela ya Kamiti Jumapili iliyopita ambapo walikamatwa wakiwa safarini kuelekea Somalia.
Kama Umependa Habari Hizi Download APP ya UDAKU SPECIAL Kwenye Simu Yako Kwa Kubonyeza >>HAPA
Mahabusu hawa waliotoroka usiku wa kuamkia leo ni Watuhumiwa wa mauaji na wizi walichimba shimo na kutoa matofali yaliyokua pembeni ya mlango wa seli na kutoroka, Mahabusu wengine wawili waliobaki seli wanasema hawafahamu wenzao walivyotoroka.