Kenya yafunga mpaka wake na Ethiopia huku mapigano yakiendelea Kaskazini mwa nchi hiyo



Kenya imefunga mpaka wake na Ethiopia kwa muda usiojulikana kufuatia mapigano katika nchi hiyo jirani.
Serikali pia imezidisha doria kwenye mpaka wa kilomita 800 ili kudhibitikuingia nchini kwa wahamiaji haramu.

Haya yanajiri wakati baraza la mawaziri la Ethiopia lilipotangaza hali ya dharura nchini kote kwa muda wa miezi sita ijayo kufuatia waasi wa Tigray kuelekea mji mkuu Addis Ababa.

Waziri Mkuu wa nchi hiyo Ahmed Abiy alitangaza hali ya dharura katika kukabiliana na kile alichokiita tishio ambalo linaweza kuisukuma nchi hiyo kusambaratika.

Hapo awali, mkutano wa dharura ulifanyika kati ya mamlaka ya Kenya na Tume ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa ili kupanga uwezekano wa watu waliokimbia makazi yao.

Wataalam wanatarajia takriban wakimbizi milioni tano kujaribu kuvuka mpaka iwapo utawala wa nchi hiyo utaanguka .

Wakenya pia wameshauriwa kuwa waangalifu


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad