Kenya Yataka Kurejeshwa Nchini kwa Mwanajeshi wa Uingereza kuhusu Mauaji ya raia wake

 


Kenya inalenga kuiomba uingeeza kumsalimisha mwanajeshi wa btaifa hilo anayedaiwa kuhusika na mauaji ya mwanamke mmoja rai awa Kenya miaka tisa iliyopita .

Waziri wa ulinzi Eugene Wamalwa aliambia kamati ya bunge kuwa serikali ya Uingereza imeahidi ushirikiano kamili.


Bw Wamalwa alisema mwili wa Agnes Wanjiru mwenye umri wa miaka 21 uligunduliwa baada ya wanajeshi wa Uingereza waliokuwa wakifanya mazoezi nchini Kenya kuondoka nchini.


Ujumbe wa serikali ya Uingereza kwa sasa uko nchini Kenya ukifanya mazungumzo na wenzao wa Kenya, lakini wamekataa maombi yote ya mahojiano na BBC.


Bw Wamalwa aliambia wabunge Jumanne kwamba alisoma ripoti ya uchunguzi iliyohitimisha kuwa Wanjiru aliuawa na wanajeshi wa Uingereza katika ardhi ya Kenya.


Aliongeza kuwa serikali ya Kenya iliwasiliana na Uingereza baada ya taarifa ya Jumatatu ya mkuu wa polisi kwamba kesi hiyo imefunguliwa tena.


Bw Wamalwa pia alisema amepata hakikisho la serikali ya Uingereza kwamba wale wanaosakwa kuhusiana na mauaji hayo, ambao alisema wanajulikana, watafikishwa Kenya kujibu mashtaka.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad