Kenya yatangaza kupiga mnada ndege 73 za mataifa haya, wanaohitaji wakaribishwa




Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini Kenya imetangaza kupiga mnada wa ndege 73 za muda mrefu, zikiwemo ndege mbili za Jeshi la anga la Somalia.



Mamlaka ya KAA imetoa wito kwa wale wanaopenda kununua ndege hizo kufika katika kituo cha maonesho kabla mwezi huu haujaisha.

Baadhi ya ndege zisizo na rubani katika viwanja vya ndege vya KAA ni pamoja na Jeshi la anga la Somalia, Jubba Airways, Jetlink, Skyward, Eagle Aviation, Prestige Aviation, Fly540, Pan Africa Airways, na Planes for Africa.

Kamanda wa Jeshi la anga la Somalia, Jenerali Mohamud Sheikh Ali (Dable Bayloot) ameiambia BBC kwamba hakuna mtu aliyeripoti kuhusu Somalia.

“Nimeona ndege za Somalia zinapigwa mnada, lakini hakuna mtu kutoka Kenya aliyeripoti kwetu,” alisema.

“Nimefika Nairobi mara kadhaa na sijaelezwa chochote”, Jenerali alisema

Jenerali Dable Baylood aliongeza kusema kuwa kuna ndege moja tu ambayo iko huko inayomilikiwa na Somalia.

Ndege hizo zimekuwa hapo kwa muda mrefu yapata miaka 30.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad