Kesi inayomkabili mke wa bilionea Msuya yaanza kwa pingamizi



Dar es Salaam. Upande wa utetezi katika kesi ya mauaji inayomkabili mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita na mfanyabiashara Revocatus Muyella umepinga kupokelewa kwa maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa kwanza.

Washtakiwa hao wanaokabiliwa na mashtaka ya kumuua kwa kusudia Aneth Msuya,  dada wa marehemu Msuya Mei 25, 2016 katia eneo la Kibada, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Maombi hayo yametolewa na mawakili wa utetezi Omary Msemo na Nehemia Nkoko baada ya shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka, WP 4707 Sajenti Mwajuma (42) kuomba maelezo yake yapokewe kama kielelezo.

Akitoa sababu za kupinga maelezo hayo Wakili Msemo amedai maelezo hayo yalichukuliwa nje ya muda kinyume na sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2009 kinachotaka mtuhumiwa kumchukulia maelezo ndani ya saa 4 tangu alipokamatwa.

Amedai mshtakiwa alikamatwa Agosti 5, 2016 na maelezo kumchukulia Agosti 7, 2016 ambapo kifungu cha 51 kinataka muda wa nyongeza kuongezwa endapo maelezo hayajakamilika.


 
Wakili Msemo alidai sababu ya pili ya kutaka maelezo hayo yasipokelewe ni kutokana na mshtakiwa kudai maelezo hayo yalichukuliwa baada ya kuteswa.

"Suala hili lilianzia mahakama ya Kisutu hata mshtakiwa alisema kuna baadhi ya sehemu zake za mwili zilikuwa na makovu,” alisema.

Sababu nyingine ya upande wa utetezi kupinga maelezo hayo, wakati mshtakiwa anachukuliwe maelezo hakupewa haki zake kisheria kinyume na kifungu cha 53(c) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.


"Haki hizo ni pamoja na kuwa na mwanasheria, ndugu au rafiki, hivyo kwa kuwa mshtakiwa hakupewa haki hii tunapinga kupokelewa kama ushahidi katika kesi hii.

Hata hivyo Wakili Nkoko naye alidai mpelelezi ni lazima wakati anamuhoji mtuhumiwa ajue amekamatwa lini ili kujua kama maelezo ya nachukulia ndani ya muda na kama yatakuja nje ya muda, ipo haja ya kupeleka maombi mahakamani ili kuongeza muda.

Alidai sababu nyingine ya kuomba mahakama isipokee maelezo hayo wakati shahidi anatoa ushahidi wake hakueleza maelezo hayo yalichukuliwa kituo gani.

Akijibu hoja hizo, Wakili wa Serikali Gloria Mwenda alidai hoja zilizotolewa na Wakili Msemo ni za kisheria hivyo anaomba Mahakama isikilize kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi.


 
"Pingamizi 1, 2 na 3 ni ya kisheria ya nahitaji mashadi wengine kudhibitisha, hivyo tunaomba mahakama yako kufanya kesi ndogo ndani ya kesi hii," amesema Wakili Mwenda.

Jaji anayesikiliza kesi hii, Edwin Kakolanya amesema kutokana na pande zote mbili kupingana kuchukuliwa kuhusu kuchukuliwa maelezo hayo, mahakama imeona umuhimu wa kufanya kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad