HATUA ya kufunguliwa kesi mahakamani, kwa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam nchini Tanzania, Paul Makonda na mtu binafsi, kumeelezwa kumeiweka mtegoni serikali na Mahakama. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Mmoja wa mawakili mashuhuri nchini, Profesa Abdallah Safari amesema, uamuzi wa kumfungulia kesi Makonda, ni kipimo tosha kwa serikali iliyopo madarakani, kwamba “inachokisema ndicho inachokitenda.”
Alisema, “…serikali imewekwa mtegoni kwenye jambo hili. Kwamba, baada ya kuwapo tuhuma kadhaa dhidi ya Makonda, itaruhusu mtu huyo kushitakiwa? Hili ni moja ya jaribu kubwa kwa serikali na Mahakama.”
Kwa nini ni jaribu kwa serikali na Mahakama. Undani wa habari hii na rejea alizozifanya wakati wa utawala wa awamu ya kwanza ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere, Soma Gazeti la Raia Mwema, toleo la leo Jumatatu, tarehe 29 Novemba 2021.