Shahidi wa pili upande wa mashtaka katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu amekutwa na ‘diary’, kalamu na simu kizimbani.
Shahidi huyo ambaye ni Askari H4323 DC Msemwa anayefanya kazi kituo cha Polisi Oysterbay amekutwa na vifaa hivyo leo Ijumaa Novemba 12, 2021 katika Mahakama Kuu ya Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi wakati akitoa ushahidi wake.
Awali, Wakili wa upande wa utetezi, Peter Kibatala alisimama mahakamani hapo na kuieleza kuwa shahidi huyo ana simu, diary na karatasi
Hivyo Wakili Kibatala aliiomba mahakama hiyo ushahidi uliotolewa akiwa chini ya kiapo ushahidi huo uondolewe katika kumbukumbu za Mahakama.
Kibatala: Vifaa anavyo tena mbele ya mabenchi mawili ya mawakili wa Serikali.
Kibatala: Baada ya kueleza hayo, shahidi alitoa simu na diary alikuwa nayo na kuchukuliwa na karani wa Mahakama.
Jaji: Umeona hivyo vifaa anavyo?
Kibatala: Nimeona shahidi tangu zamani alikuwa Emotion na alikuwa anaandika.
Kibatala: Hivyo akaguliwe.
Jaji: Unataka akaguliwe sasa hivi ? Au tuache kwanza upande wa mashtaka wamalize kutoa hoja zao?
Kibataka: Hivyo vitu akabidhi kwa ofisa wa Mahakama halafu awe chini ya ulinzi kama tunaweza kufanya hivyo.
Jaji: Sawa.
Shahidi tayari amekabidhi vifaa hivyo kwa karani wa Mahakama na upande wa mashtaka wanaendelea kutoa hoja zao kupinga maelezo ya upande wa utetezi ya kupinga barua ya Naibu Msajili iliyotolewa na DC Msemwa, kama sehemu ya ushahidi katika kesi hiyo ndogo ndani ya kesi ya msingi.
Jaji: Nimekusikia bwana Kibatala ulisimama na kuomba Mahakama kuhusiana na shahidi kuwa na diary kizimbani.
Kibatala: Tunaomba maelekezo yako kuzingatia na muda kutokana na pingamizi diary ya shahidi iwekwe hadi pale utakapotolewa uwamuzi au wenzetu kama wanao kwa kuwa amekiuka kiapo cha mahakama.
Wakili Kidando: Hata kama hilo lilitokea Shahidi alikuwa… Hatujasikia sehemu yoyote vitu hivi vikilalamikiwa vimetumiwa wakati Shahidi anatoa ushahidi wake. Hicho alichosema Kibatala tukianza kuingia kwenye zoezi hilo tu nahitaji kuwa waangalifu kitu kama simu ni kitu binafsi. Kwanini nasema ni eneo hatari anataka kuchukua kwenye simu kuna nini na kwenye diary kuna nini.
Jaji: Ulisema Shahidi ana simu na diary hujasema kama alikuwa anatumia, tukumbushane sheria kabla Shahidi ajaingia afanyiwe upekuzi.
Jaji: Diar inaweza kupekuliwa lakini kwenye simu tunaenda mbali
Kibatala: Niliarifiwa mapema na Profesa J shahidi anasoma hasa wakati anataja majina ya askari lakini wakati tunabishana hapa alikuwa na peni
Jaji: Kwenye simu naona ugumu arudishiwe lakini kwa weekend hii nendeni mkafanye research katika maeneo hayo halafu Jumatatu tutaona namna gani ya kufanya ila simu arudishiwe diary itabaki kwa mahakama.
Wakili Kidando: Nina angalizo tunapofanya zoezi hili, sio kila ombi linaloletwa mahakamani sio lazima likubaliwe.
Jaji: Naona kuna vifungu vya sheria vimetajwa lakini kafanyeni research Jumatatu mkija tuangalie linafanywa kwa sheria ipi hapa Kibatala hukuzungumza chochote.
Jaji : Naahirisha kesi hadi Jumatatu Novemba 15 kwaajili kutolea uwamuzi Shahidi nakuonya uje kuendelea na ushahidi na washtakiwa wataendelea kubaki chini ya uangalizi wa Magereza.