Kesi ya mtoto aliyefanya mtihani wa la 7 gerezani yaanza kusikilizwa



Kesi inayomkabili mwanafunzi aliyefanya mtihani wa darasa la saba akiwa gerezani, Kunde Gambija Kilulu (15) na baba yake mzazi Sayi Gisabu imetajwa kwa mara ya kwanza katika mahakama Kuu ya Mkoa wa Shinyanga iliyo kaa katika mahakama ya hakimu mkazi wa mkoa wa Simiyu.


Kesi hiyo imesomwa na mwendesha mashtaka Rehema Sakafu na kusikilizwa na Jaji Seif Mwishehe Kulita huku upande wa utetezi wa washtakiwa ukisimamiwa na wakili Samwel Lugundija.



Kesi hiyo haikuweza kusikilizwa katika mahakama ya wazi na badala yake imesikilizwa katika mahakama ya ndani.



Akizungumza na Mwananchi baada ya kesi hiyo kutajwa, wakili Lugundija amesema kuwa baada ya kesi hiyo kusomwa upande wa utetezi imetoa hoja kuiomba mahakama kubadilisha hati ya mashitaka kutoka kesi ya mauaji na kuwa kesi ya kuua bila kukusudia na hoja hiyo imekubaliwa.



"Mtoto amekiri kosa dogo na kwa mujibu wa maelezo yaliyotoka leo mahakama imeshindwa kutoa hukumu dhidi ya mtoto kwa sababu ya kisheria ambapo mahakama inasubiri taarifa ya ustawi wa jamii kuelezea hali ya mtoto katika jamii anayotoka" Amesema Lugundija.



Hukumu ya kesi hiyo inatarajiwa kutolewa Novemba 10, 2021 baada ya kuwa taarifa ya usitawi wa jamii imewasilishwa mahakamani.


Kunde Gambija Kilulu ni mhitimu wa darasa la saba aliyefanya mtihani wa Taifa akiwa katika gazeti la Bariadi mkoani Simiyu akikabiliwa na kesi ya mauaji ambapo amefaulu kwa daraja B.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad