Mwanafunzi wa Chuo Atembea na Bango Akiwataka Watu Wamsaidie Kukutana na Mwanahabari Jeff Koinange




Kevin Yator aliamua kutembea akiwa amebeba bango lililowaomba watu wamsaidie kukutana na mwanahabari mashuhuri Jeff Koinange
Yator ambaye ni mwanaufunzi wa mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha Zetech alisema anataka kukutana na mwanahabari huyo ili amsaidie kulipa karo yake
Mwanamume huyo jasiri aliwaomba watu wamsaidie kukuza kipaji chake cha uimbaji kwa kuwa ni msanii anayechipuka
Mwanafunzi wa chuo aliyetambulika kama Kevin Yator aliamua kutembea na bango na kuomba watu wamsaidie kukutana na mwanahabari mashuhuri Jeff Koinange.

Mwanafunzi wa Chuo Atembea na Bango Akiwataka Watu Wamsaidie Kukutana na Mwanahabari Jeff Koinange
Mtangazaji wa kituo cha runinga ya Citizen TV Jeff Koinange ambaye anatafutwa na Kevin Yatar ili wakutane. Picha: Jeff Koinange. TUKO.co.ke. Source: UGC
Mwanamume huyo anayesomea uanahabari katika Chuo Kikuu cha Zetech, alisema alikuwa na matumaini ya kukutana na Koinange kwa muda mrefu.

Kwenye mazungumzo ya kipekee na TUKO.co.ke, Yator alifichua kwamba ombi lake kuu kwa mwanahabari huyo aliyebobea ni kumlipia malimbikizi ya karo ya chuo kikuu.

Alidai kwamba mambo yalikwenda mrama baada ya wazazi wake kupoteza ajira na kushindwa kumudu mahitaji yake ya masomo.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad