Kiongozi wa Mapinduzi Sudan Amfuta Kazi Mwendesha Mashtaka





Kiongozi wa mapinduzi yaliyofanyika wiki iliyopita Sudan, Luteni Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, amemfuta kazi Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP), Mubarak Mahmoud kufuatia kuachiliwa huru kwa watu kadhaa wanaohusishwa na utawala wa aliyekuwa Rais wa muda mrefu Omar al-Bashir.
 

Kufukuzwa kwa Mahmoud kumekuja baada ya mamlaka ya kijeshi kuwaachilia baadhi ya washirika wa zamani wa Bashir, akiwemo Waziri wake wa Mambo ya Nje Ibrahim Ghandour.

 

Kuachiliwa kwa Ghandour na maafisa wengine wa zamani huenda kukazua tetesi za kuwa majenerali wa kijeshi bado wanaendelea kumtii Bashir aliyepinduliwa Aprili 2019 na wanaweza kuwa walihusika katika mapinduzi ya Oktoba 25.

 

Kumekuwa na mashinikizo ya kimataifa kuwashawishi viongozi wa mapinduzi kuwaachia huru wanasiasa waliokuwa kizuizini na kurejesha serikali ya kiraia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad