Klabu ya Geita Gold Kupitia kwa Afisa Habari wake Kumtaka Fei Toto na Mukoko


Klabu ya Geita Gold kupitia kwa afisa habari wake Hemed Kivuyo imethibitisha kuwa ni kweli imepeleka maombi kwa klabu ya Yanga kutaka kujua bei za wachezaji wawili wa klabu hiyo Mukoko Tonombe na Feisal Salum “Fei Toto”.
“Ni kweli kabisa hiyo barua inayosambaa mitandaoni ni ya Geita Gold ambayo tumeituma kwenda kwa Young Africans “Yanga” kuuliza bei ya wachezaji hao, unajua viongozi wa Geita Gold chini ya Mkuregenzi Zahara Michuzi pamoja na mwenyekiti, ni watu wanaoheshimu taratibu za Soka, kwa hiyo sio vyema kwenda kuongea na mchezaji ambaye anamkataba kwa hiyo tumetuma maombi kwa uongozi wa Yanga kama tunaweza kukaa kitako kuzungumza bei za wachezaji hao”. Amesema Kivuyo alipozungumza na Sturday Sports ya East Africa Radio

kwa upande mwingi afisa habari huyo amesisitiza kuwa si wachezaji hao tu wanaowawania bali wapo wengi ikiwa ni malengo ya kuboresha kikosi hicho katika dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa Disemba 15, 2021.

“Hii inadhihirisha kuwa uongozi wa Geita upo Serious na dirisha dogo pamoja na kwamba wanaamini kikosi walichonacho hivi sasa ni kikosi bora sanaa, ila wanataka wakiongezee nguvu kwa sababu nia si kubaki Ligi Kuu nia ni kugombania top 4(nafasi nne za juu) ikibidi kutwaa ubingwa”. Alisema kivuyo

Geita Gold inashiriki Ligi Kuu soka Tanzania bara kwa mara ya kwanza, na katika michezo 5 ya ligi waliocheza mpaka sasa katika muendelezo wa msimu huu wa 2021-22 wamekusanya alama 2 baada ya kufungwa michezo 3 na kutoka sare michezo 2.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad