Korea Kaskazini yafyatua mizinga kuimarisha uwezo wake





Korea Kaskazini imefanya zoezi la kufyetua mizinga ili kuimarisha uwezo wake wa ulinzi. Haya yameripotiwa leo na shirika la habari linaloendeshwa na serikali ya nchi hiyo KCNA.



Hili ni jaribio la hivi karibuni zaidi katika wakati taifa hilo linazidisha shinikizo dhidi ya Marekani na Korea Kusini kuachana na kile linachokiita sera za uadui dhidi yake.

KCNA imeripoti kuwa mazoezi ya kufyetua mizinga kati ya vitengo vilivyoandaliwa yalifanyika jana Jumamosi na kuhudhuriwa na maafisa wakuu wa serikali na jeshi.

Hata hivyo, kiongozi wa taifa hilo Kim Jong Un hakutajwa kwenye ripoti hiyo hali inayomaanisha hakuhudhuria mazoezi hayo. Mwaka uliopita, kiongozi huyo alisimamia mazoezi sawa na hayo.

Tangu mwezi Septemba, Korea Kaskazini imefanya mfululizo wa majaribio ya makombora yake mapya pamoja na silaha zenye uwezo wa nyuklia ambazo zinayaweka mataifa ya Korea Kusini na Japan ambayo ni washirika wa Marekani katika hatari ya mashambulio.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad