Kumekucha..Pochettino Kocha Mpya Man United?





MKUU wa benchi la ufundi la PSG, Mauricio Pochettino, ndiye anayehusishwa zaidi na kibarua cha kwenda kuinoa Manchester United iliyomfuta kazi Ole Gunnar Solskjaer.

Pochettino anatajwa kuwa ni kipenzi cha mabosi wa Mashetani Wekundu hao wa Old Trafford, licha ya kocha wa Ajax, Erik ten Hag, naye kupigiwa chapuo.

Wakati pia kocha wa Leicester City, Brendan Rodgers, akihusishwa, inaelezwa kuwa mambo yanaweza kwenda vizuri kwa Pochettino kwani Muargentina huyo naye ameonesha kuvutiwa na mpango wa kutua Man United.

Kwa upande wake, Ten Hag raia wa Uholanzi amesema hajasikia chochote juu ya taarifa zinazodai anatakiwa kwenda kuliongoza benchi la Man United.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad