Alichoandika mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, MB Dog…
“(Tip Top) bado ni familia bora sana kwangu kwa wakati wote, matatizo yapo na yanasababishwa na sisi binadamu kwa kukosa uelewa.
“Nilipoachana na familia hii moja ya viongozi wangu aliahidi na kuhakikisha kama wao ndiyo walinitoa basi nisubiri maumivu kwenye safari yangu ya muziki.
“Na kwa sababu nilikuwa sina kipato chochote cha moto nimekipata mpaka sasa wameshikilia (haki zangu kwa njia za panya ila hili litakwisha na litawagharimu wasipokuwa makini).
“Kwenye hili la konde hatupaswi kumlaumu sana @diamondplatnumz wala kulaumiwa @harmonize_tz , hawa vijana hawana wanalolifahamu kuhusu kiwanda cha muziki.
“Nyuma yao kuna watu ni viongozi, kumbuka hawa viongozi wana makovu na majeraha ambayo kupona kwake ni kufeli kwa dhahabu ambazo walizichimba muda mrefu na zikawatoka mikononi.
“Tip Top Connection, TMK Wanaume Family, Bongo Records, Yamoto Band, Wakali Kwanza na makundi mengine.
“Hawa watu hawawezi kuona wanashindwa kwa lolote, mimi nilipendekezwa kuingia kwenye MTV Africa Music Awards 2009.
“Hii dili iliikuja kunifikia milango ndiyo inafungwa cauz nilitakiwa kuwasilisha wasifu wangu lakini kwa sababu lilipita kwa mtu ambaye alikuwa msimamizi wangu ambaye alipata umaarufu kupitia mimi mpaka akawa hapo alipo, akaiminyia ndani.
“So nachoweza kusema mfumo wetu wa kiwanda cha muziki hasa Tanzania una matatizo makubwa, serikali yapaswa kuingilia kati, matatizo kama haya yako duniani kote lakini wenzetu sheria huwa zinafuata mkondo wake.
“Watu hawathubutu kuchezea vipaji vya watu namna hii, tumpongeze Nassibu japo anatumika vibaya kwa anachokifanya, kwani kinaleta chachu na solution ya haya yote.
“Nina mengi sana siku nikiruhusiwa kuongea na vyombo vya habari nitayaweka wazi niliowakwaza tusameheane kwa hili gazeti.”