Kuna watu huwa hawaelewi na wanamuona @diamondplatnumz kama vile Ni msanii mkubwa sana Africa, tena na yeye mwenyewe anavyovimba ndio anazidi kuaminisha mashabiki zake kwamba yeye ni mkubwa sana Africa wakati ukweli sio hivyo. Kijana bado anahatua ndefu sana katika muziki wake.
Hivi sasa Wizkid mmoja ni sawa na Diamond kumi. Suala la usiku wa kuamkia leo Wizkid kuperform show moja na Chris brown sio suala dogo, na baada ya show, Chris brown amepost kwenye instagram yake na amekubali kuwa wizkid ni moto wa kuotea mbali.
Wizkid ameperform ngoma zaidi ya Nne katika show ile, hii inaonesha kuwa anathamani kubwa sana Duniani , angekuwa Diamond angepewa dakika mbili tu.
Wizkid ameperfom Kwenye 02 Arena, London ambayo uwezo wake ni kuchukua watu 20000, Shangwe alilopata sio la Dunia hii, Daimond show zake Ulaya huwa unafanya kwenye Vilabu vya pombe.
Diamond atasubiri sana kuwa kama Wizkid, hivi sasa aendelee tu kupambana na @harmonizetz
JE UNATAKA KUNUNUA GARI JIPYA/USED, KUUZA GARI LAKO, KUAGIZA GARI KUTOKA NJE YA NCHI, WACHEKI @nyonimagari Wawezeshe Kirahisi sana Jambo lako.