MAC Voice "Nilijiona Kama Ninaota Kusainiwa na Rayvanny"




“Mmmh siri ya mwezi…Siri ya nyota, siri ya angani…Siri ya njozi usingizi…Siri ya kitandani…Ila siri ya penzi, siri ya moyo…Siri ya nani?..Siri ya chozi ni maumivu ndani kwa ndani…“Mapenzi niliyaanzisha yakanifurahisha…Yakanibadilisha jamani…Na siyo tu kumridhisha…Nikamdhaminisha, nikamtamulisha nyumbani…Sasa leo yamekwisha yananidhalilisha…Yananiaibisha hadharani…Ila yote ni maisha, japo nahuzunika…Eeh wa kuninyamazisha ni nani?..Sijuti kukufahamu, ila najuta kukuamini…Kasuku ndege wangu leo umekuwa bundi…Pokea zangu salamu, bado sijui nitapona lini?Umevunja moyo yangu, we ndo ulikuwa gundi…“Ile siku unafungasha mabegi…Ulidondosha picha yako dondo…Ndo najilazia kwa bedi…Aki ya Mungu umenipiga zongo…Naomba msalimie shemeji…Aki ya nani amepata chombo…Na kama ukiskia nimededi…Jua ni mawazo msongo…Nenda, salama nenda…Nenda, salama nenda…Nenda, salama nenda…Nenda, salama nenda…”Hii ni sehemu ya mashairi ya Ngoma ya Nenda ya msanii nayekuja kwa kasi kunako anga la muziki mtamu wa Bongo Fleva,.


NI msanii kutoka kwenye lebo inayosumbua vichwa vya habari kwa sasa ya inayomilikiwa na mtoto wa Kinyakyusa, Raymond Mwakyusa au Rayvanny.

Unaambiwa licha ya kuwa kwenye gemu kwa kipindi kifupi, mwamba huyu mwenye umri mdogo, lakini anafanya mambo makubwa.


Tayari amefanya maajabu ya kutosha huko mjini YouTube na kitaani pia kwa kuachia EP yenye ngoma kali kama zote.


Miongoni mwa ngoma kali alizofanya na zikampa jina kwa sasa akiwa zao la Next Level ni pamoja na Kama aliyoshirikiana na bosi wake, Rayvanny.Pia kuna Tamu, Nenda, Bora Peke Yangu, Mama Mwenye nyumba, Nampeda na nyinginezo.Gazeti la


IJUMAA limepiga mastori na Mac Voice akiwa kama staa mpya kwenye gemu ambapo anafunguka mambo kibwena;


IJUMAA: Umeweza kufikisha streams milioni 5 kwenye EP yako ndani ya muda mfupi, hongera kwa hilo…


MAC VOICE: Ahsante sana pia naahidi nitazidi kupambana siku hadi siku.

IJUMAA: Hogera kwa kuwa msanii wa kwanza kusajiliwa Lebo ya Next level…


MAC VOICE: Ahsante sana, nashukuru.



IJUMAA: Mashabiki wange-penda kufahamu msoto uliopitia hadi kufikia hapa ulipo…

MAC VOICE: Kwa kweli msoto upo sana tu, naweza nikasema hivyo ila kwa upande wangu mimi huwa sipendi sana kuongelea mambo yalipita kwa sababu naona yatakuwa hayana maana sana ila kikubwa ni kuwapa moyo wale wengine ambao bado wanapambana kwenye gemu.


IJUMAA: Ulijisikiaje ulipotangazwa kuwa msanii wa lebo hiyo?

 

MAC VOICE: Nilijisikia faraja, niliona kama nipo kwenye ndoto, ilinichukua kama wiki nzima siamini yaani kilichotokea.

 

IJUMAA: Ushirikiano wako na wasanii wenzako kutoka kwenye lebo ya ya jirani ya Wasafi ukoje?

 

MAC VOICE: Kwa kweli tunaishi kama familia kabisa na ninashukuru Mungu kuwa miongoni mwa familia hiyo.

 

IJUMAA: Wamekupokeaje?

 

MAC VOICE: Kwa upendo wa hali ya juu, najisikia faraja, naona kama ndoto zangu zinakamilika.

 

IJUMAA: Unajisikiaje kufanya kazi na Rayvann?

 

MAC VOICE: Vizuri sana, tena zaidi ya sana maana nafanya kazi kwa uhuru.

 

IJUMAA: Ni mtu wa aina gani kwako?

 

MAC VOICE: Ni zaidi ya kaka kwangu, namkubali sana na kila siku namuombea dua za mafanikio juu yake.IJUMAA: Ni kitu gani ambacho amekibadilissha kwenye maisha yako?

 

MAC VOICE: Amenifanya nimejulikana kwa haraka mno kwa hilo namshukuru sana, Mac voice sasa ninaheshimika.

 

IJUMAA: Utaratibu ukoje, labda kuna mkataba wowote ambao umeusanini Next Level?

 

MAC VOICE: Hilo kwa kweli siwezi kulijibu ni swali la uongozi wangu.

 

IJUMAA: Kufanya kazi na Rayvanny inakupa ugumu gani?

MAC VOICE: Naona hakuna ugumu wowote kwa sababu ni mtu peace (mtu mwenye amani).

 

IJUMAA: Hizi ngoma ambazo unazifanya unatunga mwenyewe au ni kaka mkubwa anakupa sapoti?

 

MAC VOICE: Natunga mwenyewe.

 

IJUMAA: Kwa sasa
wanasema kwamba Mac Voice mmoja ni sawa na wasanii wote wa Lebo ya Konde Gang, je, unadhani ni kweli?

 

MAC VOICE: No comment.

 

IJUMAA: No Comment ndiyo nini, ina maana huna uwezo wa kuwapita? MAC VOICE: Ukweli ni kwamba mimi sina cha kuzungumza juu ya hilo, hawa ni mashabiki wameongea mimi nipase kusema tu kwangu kazi ndiyo zinaweza kuongea.

 

IJUMAA: Unajiona kwenye levo gani miaka michahe ijayo?

 

MAC VOICE: Najiona Mbali sana kwa kweli ila Mungu ndiye muweza wa kila kitu

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad