Baada ya Jina la msanii macvoice kuonekana katika nominations za tuzo za @aeausa , kumeibuka mijadala mikubwa, kwamba kwanini jamaa ana mwezi mmoja tu kwenye game lakini ameanza kuwa nominated katika moja ya tuzo kubwa Africa na Dunia kwa ujumla.
Msanii huyu kutoka NLM-Lebo ya @rayvanny amepata nomination katika category ya Best Upcoming artist in Africa, Msanii bora anayechipukia Barani Africa.
Je macvoice anastahili kukaa kwenye hiyo nafasi, au hastahili kabisa, amebebwa tu?
Tujikumbushe tu, Macvoice ndani ya mwezi mmoja tu kwenye game amepata mafanikio makubwa sana, ambayo wasanii wengi hawajawahi kuyapata.
Ndani ya mwezi mmoja EP yake imefikisha jumla ya Streams zaidi ya Million 4 katika platform ya Boomplay.
Amewahi kuwa msanii watatu kati ya wasanii 100 wanaofanya Vizuri BOOMPLAY.
Amefanikiwa kupata 90k+ Youtube Subcribers pamoja na 100k+ Instagram Followers.
Anajumla ya views zaidi ya million 4 katika platform ya Youtube.
Ndani ya mwezi mmoja tu, tayari Ameanza kupata booking za shows.
Mwezi October ameingia katika Top Ten ya wasanii wa Tanzania Waliotazamwa sana Youtube.
Anajumla ya streams Zaidi ya Mil 10 katika platform kubwa za muziki (SPOTIFY, , BOOMPLAY, AUDIOMACK, ITUNE).
Kwa hizi Data, je bado hastahili tu kukaa kwenye Category moja na Omahlay, Guchi, Liya, Ruger na wengine kadhaa ili kugombania tuzo ya msanii bora chipukizi katika Bara la Afrika?
Vipi kuna uwezekano MacVoice kushinda tuzo hii, amshinde Omahlay, Guchi, Ruger na wengineo?