MSEMAJI wa Klabu ya Yanga, Haji Manara ameokoleza kile kinachoelezwa kuwa timu hiyo iko kwenye harakati za mwisho za kumsajili nyota wa kimataifa wa Zambia Clatous Chama kutoka Berkane FC ya Morocco.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara ameandika; “Nchi tuisimamishe sasa hivi au baadae? Dadadeki, Ok biashara tushamaliza na hapa Eng. Hersi ndio anashughulikia ATC, oooh sorry ITC.😅😅
Jana mliongopewa nn vile?
We Are Yanga, The Home of Champions.👌 Sijui nifanye Press au niseme humu humu, halafu wala haturingi🤪🤪”
Vijembe hivi vya msemaji huyo machachari vimetafsiriwa kuwa labla huenda tayari nyota huyo amefanya mawasiliano na Yanga SC baada ya kuripotiwa kutokuwa na furaha nchini Morocco.