Mange Kimambi Awasanua Tena Wasanii Bongo "Wasanii wa Bongo AMKENI Mtakufa Maskini..Redio ziwalipe Wakicheza Nyimbo ženu"


Wasanii wa Tanzania, inabidi muamke na muwe kitu kimoja la sivyo mtakufa maskini.

Haki ukiangalia followers wa wasanii wa Tz na wasanii wa Nigeria wasanii wa Tz mna followers wengi ila hamna kitu mko maskini. Why??

Hivi mnajua nchi za nje kwa mfano hapa marekani TV na radio zinalipa $6 kila wanapopiga nyimbo ya msanii?? Yani kwa hapa marekani kuna kitengo kimewekwa kila mwezi radio zinawakilisha kwenye hicho kitengo nyimbo zooote walizopiga na mara ngapi walizipiga then wanatumiwa bili na hiko kitengo then radio zinalipa pesa kwenye kitengo then hiko kitengo ndo kinafikisha pesa kwa wasanii wenye nyimbo zao. Ila marekani ni tofauti kidogo na nchi zingine. Hapa marekani anaelipwa ni mwandishi wa Ile nyimbo. So kama msanii aliandikiwa nyimbo hela hatopokea atapokea aliendika kama aliandika yeye atalipwa yeye.

Ila Tanzania eti wasanii ndo wanalilia kupigiwa nyimbo zao tena sometime wanalipa zipigwe 🤦🏽‍♀️. Jamani inabidi muelewe kuwa bila nyimbo zenu hakuna radio itakayo survive. Nyinyi ndo mnaowafanya wanapata wasikilizaji. Inabidi muanze kulipwa kwa kila nyimbo zenu zinapopigwa na media.

Na nawarudia tena acheni kufanya interview za bure ndo maana mnabaki maskini. Mtu unaenda kumwaga Siri zako kwenyw bureeeeeeee. Hivi una akili kweli? Unatakiwa ulipweeee.

Acheni kutajirisha watu huku nyinyi mnakufa maskini. Lazma kuwe na win-win situation kila mtu awin. Sasa nyie mnawatumikia watu bure, yani mnadhani mnafanyiwa favor. Amkeni please. Nyie ndo mnawafanyia favor.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad