Maombi Ya Vibali vya Kazi Kwa Raia wa Nje Sasa Ndani Ya Saa 24




WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, amesema miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania, ofisi hiyo imeweza kusimamia na kuboresha mfumo wa kieletroniki wa kushughulikia maombi ya vibali vya kazi kwa raia wa kigeni.


Akizungumzia mafanikio ya Wizara hiyo, Waziri Jenista Mhagama, amesema mfumo huo umepunguza muda wa kushughulikia maombi ya kibali kutoka siku za kazi 14 zilizopo kisheria hadi siku saba.



Amesema kutokana na kupungua kwa hatua za uombaji wa kibali kutoka hatua 33 hadi hatua tatu pekee.



Aidha, amesema mfumo huo, umeunganishwa na mfumo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) na inategemewa Taasisi nyingi zaidi za Serikali zitaendelea kuunganishwa na Mfumo huu.



Mafunzo kuhusu utumiaji wa Mfumo yametolewa kwa watendaji wa ndani na nje ya Serikali. Aidha, mfumo umeimarisha uwazi na uwajibikaji, kupunguza urasimu na vihatarishi vya rushwa katika kushughulikia vibali.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad