Wimbi la wasanii tokea Nigeria kuja kufanya show kwenye nchi za watu wengine hasa Afrika Mashariki,na mbaya zaidi wasanii wazawa wakiwa hawapewi thamani kama wanavyopewa wasanii hao, imezidi kuwakata wasanii wengi tu. Inaeleweka wazi kinachofanywa na @ericomondi hivi sasa, Lengo si kukataza show za wapopo nchini mwao,lengo ni kuweka value sawa na wasanii wazawa.
Ishu hii imemfanya msanii @jchameleon amuunge mkono Eric Omond Licha ya wasanii wa Kenya kumkataa, Jose Chameleon mwaka 2017 aliwahi kataa kuperform kwenye show kubwa jijini Kampala baada ya bango la show (Billboard) kuweka picha kubwa ya Wizkid na kipicha kidogo cha J. Chameleon, hii ilitafsirika kama ni kitendo cha dharau kwa wasanii wazawa.
Ishu hii pia imefika mezani kwa King Bad, @marioo_tz ambaye ameonyesha kumuunga mkono Eric Omondi na kuonyesha masikitiko kwa hadi kaka zao kwenye hii game kuwasapoti zaidi maunderground wa Nigeria kuliko kuwainua wasanii wao,
Majibu mengi ya promoters tokea Bongo lakini hata Kenya, yamekuwa ni Muziki ni Biashara, lazima wanapoandaa show waangalie je hela iliyowekwa kwa msanii fulani itarudi. Wakikiri kuwa show za Wanaijeria zinarudisha pesa kuliko show za Wabongo/wakenya.