Mashabiki wa Mpira Wana Hatari Kubwa ya Kupata Shambulio la Moyo


Kwa mujibu wa Utafiti wa Chuo Kikuu Cha Oxford uliofanywa kwa mashabiki wa timu ya taifa ya Brazil mwaka 2014 kabla na baada ya mchezo wake na Ujerumani wakati wa kombe la dunia, ulionesha kuwa kiasi cha vichocheo vya cortisol viliongezeka sana kwenye mate yao. Hii ni baada ya kupokea kipigo kizito cha magoli 7-1.

Vichocheo vya cortisol vinapozalishwa kwa wingi mwilini vinaweza kusababisha mishipa ya damu ipungue ukubwa wake, shinikizo la damu liongezeke pamoja na kuongeza udhaifu kwenye kuta za moyo kwa watu ambao tayari mioyo yao inakabiliwa na magonjwa mbalimbali. Athari hizi zinaweza kwenda mbali zaidi kwa kusababisha hisia za mtu kujihisi hayupo salama hivyo maisha yake yapo hatarini.

Utafiti huu unaelezea kuwa, watu hawa huwa na hatari kubwa ya kupatwa na shambulio la moyo, na wanaweza kupoteza maisha ikiwa mihemuko ya hisia zao haitashughulikiwa vizuri na wao wenyewe, pamoja na jamii inayowazunguka.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad