Matokeo ya mtihani uliovuja yafutwa nchi nzima





Mganga Mkuu wa serikali Dkt. Aifello Sichalwe, amesema kuwa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limefuta matokeo ya mitihani ya nadharia (theory) kwa masomo yote ya programu ya utabibu ngazi ya tano (NTA Level 5) baada ya mitihani hiyo kuvuja.


Dkt. Sichalwe amesema kuwa baraza hilo pia limeagiza kurudiwa kwa mitihani hiyo upya ndani ya wiki sita kuanzia Novemba 1, 2021, huku akisisitiza Baraza limeagiza mitihani hiyo ifanyike sambamba na mitihani ya marudio (Supplementary Examinations) kwa programu zingine za afya nchi nzima.



Dkt. Sichalwe amesema, Wizara imesikitishwa na tukio na itaendelea kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili kukamilisha uchunguzi na kuwachukulia hatua wale wote walioshiriki kufanya udanganyifu huo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad