Meya mteule wa New York ataka kulipwa mshahara kwa Bitcoin





Meya mteule wa New York City Eric Adams, amesema angependa hundi zake tatu za kwanza yawe kwa fedha za mtandaoni, bitcoin.


Kapteni huyo wa zamani wa polisi alichaguliwa wiki hii kuchukua wadhifa huo mwishoni mwa muhula wa meya Bill de Blasio mwezi Januari.



Bw Adams alisema kwenye mtandao wa kijamii kwamba alitaka kuashiria nia yake ya kuifanya New York kuwa "kitovu cha soko la sarafu za kidigitali".



Thamani ya bitcoin, ambayo ni kubwa zaidi duniani, imekuwa tete sana, tangu ilipoundwa mwaka wa 2009.



Kauli ya Bw Adam inaonekana kuwa jaribio la kumpikumeya wa Miami, Francis Suarez, ambaye tayari alikuwa amesema katika ujumbe wake wa Twitter kwamba atachukua hundi yake ya kwanza ya malipo kwa bitcoin, baada ya kuchaguliwa tena.



Bwana Suarez tayari amesema angependa kuanzisha Miami kama kitovu cha sarafu za digitali



Bw Adams alizidisha dau hilo kwa kuomba malipo ya miezi mitatu kwa njia hiyo.



Mnamo Agosti Bw Suarez alisaidia kuanzisha sarafu hiyo inayoitwa MiamiCoin inayoendeshwa na shirika lisilo la faida, CityCoins.



Inatuma 30% ya thamani ya sarafu ambayo inaundwa kwenye kompyuta ya mtu hadi jiji na imechangisha $7m jijini Miami, kwa mujibu wa Washington Post.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad