Mfanyakazi wa Muhmbili Afariki Akivuta Kamba




Mfanyakazi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Ally Lidengi amefariki uwanjani wakati akicheza mchezo wa kuvuta kamba kwenye mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Taasisi za Umma na sekta binafsi (SHIMMUTA) ambayo yanaendelea mjini Morogoro.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu hospital ya Taifa Muhimbili Daktari Prakseda Ogweyo amesema tukio hilo limetokea juzi Novemba 20,2021 katika Uwanja wa Jamhuri Morogoro ambapo amesema marahemu huyo baada ya kuvuta kamba alianguka na alikimbizwa Hospitali ya Rufaa Morogoro tayari alikutwa ameshafariki

Amesema kwa sasa mwili wa marehemu unasafrishwa kuelekea hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi wa chanzo cha kifo chake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad