Mhudumu wa hospitali akiri kuibaka miili ya wafu 100 ndani ya miaka 12




 
Muhtasari

Tahadhari: Taarifa hii inaweza kuwa na maneno makali kwa baadhi ya wasomaji.

Mhudumu katika hospitali nchini Uingereza alikiri kuwauwa wanawake wawili mwaka 1987 na kubaka miili ya wafu wa kike 100 , wakiwemo watoto

Katika siku ya kesi ya mauaji iliyofanyika katika mahakama ya eneo la Maidstone Crown Court, Fuller aligeuza kilichotarajiwa kuwa kukubali au kukana mashitaka na kuwa kutubu.

Awali alikiri kuibaka miili ya wafu katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Kent kwa kipindi cha miaka 12.


 
Awali Bw Fuller alikuwa amekiri kuwauwa wanawake, akisema madai yalikuwa "sio ya uwajibikaji ", lakini akakana binafsi kuwauwa.

Jaji Cheema Garb aliliagiza jopo la mahakama kumtia hatiani kwa kuwauwa wanawake hao wawili baada ya kauli yake.

Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza Preeti Patel alisema, " Kesi hii ni mbaya sana. Uhalifu unaoumiza uliotekelezwa katika kesi hii utasababisha maumivu na kuwasumbua watu kiakili.


Nataka kuchukua fursa hii kuwakumbuka wasichana hawa, Wendy Nell na Caroline Pierce, ambao maisha yao yalikatizwa miaka 30 iliyopita.

Nina matumaini kuwa familia zao zitapata faraja na ahueni katika upatikanaji wa haki katika kesi hii.

Kabla ya kesi , Bw Fuller alikuwa amekiri makosa 51, yakiwemo makosa 44 dhidi ya waathiriwa 78 waliotambuliwa katika vyumba viwili vya kuhifadhia maiti ambako alifanya kazi kama fundi wa umeme.

Familia ya Bi Neil ilisema katika taarifa yake kwamba : "Ni vizuri kujua kwamba sasa yuko nje ya mahali ambapo anaweza kuumizwa na yeyote ."


 
Wapelelezi katika kesi hiyo wanasema ushahidi uliokusanywa hivi karibuni baada ya kuendelea kwa kesi, kama vile kipimo cha DNA, na operesheni kubwa ya polisi iliyogarimu pauni milioni 2.5 imepelekea Bw Fuller kupatikana na hatia ya mauaji mara mbili.

Kulingana na uchunguzi huo mate na vinasaba vingine-DNA-vilipatikana kwenye kitanda cha Bi Nile, taulo na ushahidi mwingine wa kingono. Sampuli za vielelezo vya ngono pia zilipatikana kwenye suruali za 'tights' ya Bi Pierce.

Zilikuwa ni nguo pekee alizokuwa amevaa mwilini mwake wakati ulipopatikana kwenye mtaro wiki tatu baada ya kutekwa kwake.

Msako uliofanywa katika nyumba ya Bw Fuller baada ya kukamatwa kwake kuhusiana na mashitaka ya mauaji ulibaini kuwa alikuwa ametunza picha za ajabu za utupu na video za mamilioni ya watoto katika mojawapo ya vyumba vya nyumba yake .


Alikuwa amezihifadhi picha hizi za aibu katika , floppy disks, DVDs na memory card nyingi.

Bw Fuller amekuwa akifanya kazi kama fundi wa umeme katika hospitali mbali mbali tangu mwaka 1989, na alikuwa amefanya kazi katika hospitali za Kent na Sussex hadi zilipofugwa Septemba 2011.

'Ni uhalifu wa ambao haukuwahi kutokea kabla'

Kitendo cha Fuller cha kuwakosea heshima maiti ni uhalifu ambao polisi ya Kent, au kikosi chochote cha Uingereza hakijawahi kukumbana nao kabla.

Kwa zaidi ya miezi minane iliyopita , msaada maalum wa thamani ya pauni milioni 15 1.5 kwa ajili ya waathiriwa umeundwa kwa ajili ya kesi hii na unawahusisha polisi 150 waliopewa mafunzo maalum ya kukabiliana na uhalifu wa aina hii.


 
Mahakama ilisema kulikuwa na ushahidi kwamba Bi Neil alibakwa baada ya kifo chake au wakati aliposhambuliwa. Bi Neil aliuawa tarehe 23, 1987, katika nyumba yao iliyopo kwenye eneo la barabara ya Guildford.

Katika taarifa iliyotolewa baada ya ombi lililotolewa na Full, familia ya Neililisema kuwa ilitaka kujua kwa miaka 34 ni nani aliyemuua na ''hali yake katika muda wa mwisho kabla ya kifo chake ."

"Sasa tunajua," ilisema taarifa yao, na kuongeza kwamba wanasikitika kwamba ilikuwa mbaya kuliko walivyowahi kufikiria'' , ilieleza taarifa hiyo.

"Tuna matumaini kuwa tunaweza kuomboleza na kupona ," iliongeza na kwamba .Na sasa mnaweza kuanza kumkumbuka kama msichana mrembo, mkarimu, na mwenye kujali watu''

Ni taarifa chache sana zinazofahamika kuhusu kilichotokea kwa Bi Pierce baada ya kutekwa nje ya nyumbani kwao katika eneo la Grosvenor Park Nobemba 24. Majirani waliripoti kusikia mayowe, lakini mwili wake ulipatikana katika shamba moja na mfanyakazi wa shamba hilo Romney Marsh, maili 40 kutoka nyumbani kwao.

Polisi inasema kuna uwezekano mkubwa kwamba Bw Fuller alikutana na wasichana hawa wawili kabla ya kuwauwa . Filler Supa Snap alikwua mteja wa kampuni ya kupiga picha ambako Bi Neil alikuwa akifanya kazi.

Picha zilizokamatwa kutoka kwa Fuller pia zinanyesha kwamba Fuller pia alikuwa akitembelea mgahawa wa Brown ambako Bi Pierce alikuwa akifanya kazi kama Meneja.

kujali watu''.

Ni taarifa chache sana zinazofahamika kuhusu kilichotokea kwa Bi Pierce baada ya kutekwa nje ya nyumbani kwao katika eneo la Grosvenor Park Nobemba 24. Majirani waliripoti kusikia mayowe, lakini mwili wake ulipatikana katika shamba moja na mfanyakazi wa shamba hilo Romney Marsh, maili 40 kutoka nyumbani kwao.

Polisi inasema kuna uwezekano mkubwa kwamba Bw Fuller alikutana na wasichana hawa wawili kabla ya kuwauwa . Filler Supa Snap alikua mteja wa kampuni ya kupiga picha ambako Bi Neil alikuwa akifanya kazi.

Picha zilizokamatwa kutoka kwa Fuller pia zinanyesha kwamba Fuller pia alikuwa akitembelea mgahawa wa Brown ambako Bi Pierce alikuwa akifanya kazi kama Meneja.

Fuller pia alirekodi visa 30 vya wizi katika miaka ya 1970, ambavyo polisi waliviita "creeper style.". Lakini hakuwahi kufungwa kwasababu uhalifu wake haukuwa na ushahidi wa polisi wa hifadhi ya data za DNA za polisi.

Waziri wa afya wa Uingereza Sajid Javed, amesema kuwa Huduma za afya za Uingereza zimeandikia barua hospitali zote kukagua vyumba vya maiti na kutathmini taarifa za uchunguzi wa mait kufuatia kesi hii.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad