Matumbo yetu yataweza kuhimili vyakula bandia vya maabara?




Wakati dunia ikiwa katika mjadala mkubwa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi hasa kutokana na mkutano wa kilele wa hali ya hewa wa COP26 unajumuisha viongozi wa dunia kule Glasgow, wataalamu wa teknolojia ya chakula wanajitahidi kutafuta jawabu la protini mbadala na namna zinavyoweza kutumia katika vita dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa.


Watafiti katika nchi nyingi wanatafuta mbadala ya nyama (kama chanzo kikuu cha jadi cha protini kwa sasa) kwa kuwa mifugo ni moja ya sababu za ongezeko la joto duniani.



Wazo la protini mbadala linaungwa mkono hata na nyota wa filamu za Hollywood - Leonardo DiCaprio. Lakini ni wapi, kwa mantiki hii sasa ni wapi walipoamua baadhi ya wawekezaji wakubwa wa Ulaya kuwekeza fedha zao?



Fikiria maeneo makuu matatu ya biashara ya vyakula mbadala vya mimea ikiwemo hizi za kshangaza: kuzalisha vyakula maabara na kuprinti vyakula kupitia printa maalumu.





Mnamo Desemba 2020, Singapore ilikuwa nchi ya kwanza ulimwenguni kuanza kuuza nyama inayozalishwa katika maabara.



Kwa maneno rahisi, teknolojia hiyo iko namna hii: wanasayansi huchukua seli kutoka kwa misuli ya mnyama au tishu za 'adipose' na kuzipandikiza maabara katika mazingira rafiki ya ukuaji .



Kampuni ya 'Eat Just now' yenye makao yake huko San Francisco Marekani yenyewe inauza nchini Singapore kuku waliozalishwa kwenye maabara.



Hii ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa usalama wa nchi, unaolenga kupunguza utegemezi wa kuagiza chakula kutoka kwa majirani zake.





Ni nini kinazuia nchi zingine kufanya vivyo hivyo?

Kwa baadhi ya nchi ni jambo gumu kupata kibali kutoka kwenye mamlaka za udhibiti ili kutengeneza vyakula bandia ikiwemo nyama, anaelezea Carsten Gerhardt, kutoka AT Kearney, kampuni ya ushauri kwenye masuala ya chakula na kilimo.



Ingawa katika baadhi ya nchi , sula hilo ni rahisi zaidi kuliko nchi nyingine. Uholanzi kwa mfano iko mstari wa mbele katika teknolojia ya nyama ya vitro. Kwa hiyo, wachambuzi wanatarajia kuwa katika miaka michache ijayo, wazalishaji wa nyama bandia ya Uholanzi, Moas Meat and Meatable watajaribu kupata kibali kutoka kwa wasimamizi wa Umoja wa Ulaya, ili kuzalisha kwa wingi na kuuza Ulaya nyama hiyo ya maabara.



Lakini hatua kubwa zaidi zinatarajiwa kuchukuliwa na wazalishaji wa Marekani, Memphis na New Age Meats, ambayo ina mkono wake kwenye taasisi ya Bill Gates.



Hata hivyo, hiki sio kikwazo pekee katika kupanua biashara ya uzalishaji wa nyama za aina hii, kwani ukuzaji wa nyama kwenye maabara ni mchakato wa polepole na unaotumia nishati.



Uzalishaji wa nyama bandia hutegemea seramu ya ng'ombe wa fetasi (FBS), iliyotengenezwa kutoka kwa damu ya ndama ambao hawajazaliwa, hiki ni kiungo bora cha virutubishi kwa kurutubisha nyama kwa sababu ina protini muhimu na vitamini zinazohitajika na seli kudumisha afya na utulivu.



Hata hivyo, wanasayansi wa Uholanzi walilazimika kutumia FBS na vifaa vingine vya asili ya wanyama katika mchakato wao wa kutengeneza nyama bandia.



"kwa sababu za kimaadili, na pia kwa sababu FBS ni ghali sana, hatukuweza kuzalisha nyama kwa kiwango kikubwa kwa kutumia gharama nafuu. Kwa hivyo, tumeunda njia yetu ya virutubishi bila kutumia viungo vya asili ya wanyama," msemaji wa Mosa alisema.





Tafiti mbili tofauti zilizotoka mwaka huu zimeonyesha kuwa gharama ya nyama bandia inaweza kupunguzwa ifikapo 2030 ili kushindana na nyama ya kawaida. Na kufikia 2040, tasnia hii inaweza kufikia hadi 35% ya soko la nyama duniani.



Ripoti kadhaa zinaonyesha kuwa nyama inayokuzwa katika maabara inaweza kuwa na matokeo chanya kwa mazingira - uzalishaji mdogo na matumizi kidogo ya ardhi na maji kuliko kilimo na ufugaji wa jadi.





Hata hivyo, utafiti wa hivi majuzi wa wanasayansi wa Marekani unaonya kwamba faida hizi zinahitaji matumizi makubwa zaidi ya nishati, kwani mchakato mzima unaondoka kutoka kwenye kilimo na ufugaji na kwenda kwenye viwanda.



Swali ni ni kiasi gani bidhaa za nyama zinatengenezwa maabara zitawavutia watumiaji, anasema Cyril Philott, mwanamkakati wa chakula duniani kutoka Rabobank. Kuna mambo mengi: "ladha, muonekano, gharama na urafiki wa mazingira." Hatua muhimu itakuwa ni kupitishwa kwa bidhaa za mseto, anaongeza Philott.



Bidhaa mseto ni mbadala wa nyama iliyotokana na mimea ambayo ina viambato vilivyokuzwa katika maabara kama vile mafuta.



Ikiwa watumiaji wanakubali bidhaa hizi, anaamini, maendeleo ya chakula cha bandia yanaweza kuharakishwa.



Ku 'printi' nyama (baga)

Kampuni kadhaa kwa sasa zinafanya kazi ya kutengeneza vichapishaji 'printers' vya 3D ambazo zitakuwa na uwezo wa "kupika" chakula cha jioni kwa kuvichapisha kutoka kwa tabaka nyembamba na kuzichapisha kupata tabaka nene na kubwa. Ni kama unavyochapisha ama unaprinti karatasi , unavyoweza kupata nakala hata 100 kutoka kwenye nakala moja tu ya karatasi, ndivyo itakavyokuwa kwa mashine hizi za kuprinti chakula.



Badala ya kutumia wino, watafiti hawa wanatumia vidonge maalum na viungo mbalimbali ili kupata chakula chako kwa wingi.



Printa zinazotengeneza chapati, lamba lamba 'ice cream' na vitu vingine vitamutamu kama pipi na chokoleti tayari zimepata umaarufu katika maduka makubwa Ulaya.





Lakini hivi karibuni, kulingana na wanasayansi, uchapishaji wa 3D wa 'bioprinting' utaleta mapinduzi katika uhandisi wa kibaiolojia na kuzaliwa upya kwa tishu - kama vile 'bifu ya nyama ya ng'ombe.



Teknolojia ya Microextrusion imekuja na uchapishaji tata wa protini za mboga katika matabaka, ambazo hugeuka kuwa kipande kikubwa cha nyama ikiwa na ukubwa wa kutosha na muonekano ule ule wa nyama ambapo unaweza kuikata kwa kisu kama unavyokata steki ya kawaida.



Mnamo mwezi Februari, kampuni ya Israeli ya Aleph Farms ilichapisha nyama ya kwanza ya samaki ya maabara iliyotengenezwa kwa njia hii. Kampuni hii imeunda mbinu ambayo inaruhusu aina tofauti za seli kukua katika sehemu moja.



Wanasayansi wanahitimisha kwa kusema kwamba majaribio ya chakula hayana kikomo.



Uchunguzi katika nchi kadhaa umeonyesha jinsi ya kuboresha ladha na muundo wa vyakula, kupunguza mafuta au kuongeza vitamini na vitu vingine ili vyakula visiharibike kwa wakati.



Hata hivyo, wasimamizi katika nchi nyingi wako waangalifu sana kuhusu hili, kwani athari ya muda mrefu ya uvumbuzi huu wote bado inatiliwa shaka. Wanaendelea kujiridhisha.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad