Mrembo Aliyejioa Sasa Ajipa Talaka Baada ya Kupata Mwanamume wa Kumuoa
Baada ya kufanya harusi na kujioa katika Kanisa la Sao Paulo. Picha: CO Press. Source: UGC
Harusi yake ilifanyika Septemba 2021, huku akibadilisha viapo vya ndoa baina yake mwenyewe.
Daily Star inaripoti kuwa mwanamitindo huyo wa Instagram, sasa anataka kujitaliki akiwa na matumaini ya kuolewa na mpenzi wake mpya.
Wakati wa harusi yake, Galera alifichua kuwa aliamua kujioa baada ya kuchoshwa na kuvunjwa moyo na wanaume mara nyingi.
Aliongeza kwamba aliamua kukumbatia upweke na hapana lolote la ajabu kukosekana kwa bwana harusi katika siku yake ya harusi.
Baada ya kubadilishana viapo vya ndoa, Galera alipaga akiwa mwingi wa furaha nje ya Kanisa Katoliki la Sao Paulo, nchini Brazil na koja la maua mkononi.