Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imekamata mtambo wa kuvuna maji kwa ajili ya umwagiliaji shamba la Hekta 50 katika kitogoji cha Kidozero wilayani Kibaha.
Mtambo huo unaweza kuvuna maji lita milioni moja kwa saa hali ambayo inafanya maji mengi kushindwa kufika katika kidakio cha Ruvu Chini.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa kuangalia chanzo cha maji cha Mto Ruvu Afisa Maji Bonde la Wami/Ruvu Dar es Salaam Halima Faraji amesema katika mazingira hayo wiki moja ya Novemba 12 walifika hapo na kukuta mtambo wakauchukua na kulipa faini lakini wameweza kufunga mtambo mwingine.
Faraji amesema juhudi zinazofanyika ni kwa ajili ya kuhakikisha maji hayapotei katika mikono ya watu ili sehemu za vidakio vinapata maji ili kupunguza makali ya mgao hasa kidakio cha Ruvu Chini inayolisha Bagamoyo na sehemu ya Dar es salaam.
Faraji amesema kuwa mwenye shamba hilo hana kibali cha bonde pamoja na kuchukua maji hayo ndani ya mita 60 kutoka kingo za mto Ruvu.
Aidha amesema katika uvunaji wa maji hayo anavuna masaa nane kwa nyakati za Asubuhi na Jioni huku mafuta yanayosukuma mtambo huo yakitiririka kwenye mto ambao unatumiwa na watu wengine kabla hayatiwa dawa.
Aliongeza kuwa kwa kipindi hiki wananchi waache kuvuta maji wakikutwa wakiwa na mashine na wao wenyewe wanaowakamata ili sheria ishike mkondo wake.
Hatuweza kuwaacha wananchi ambao wanapata elimu ya utunzaji wa vyanzo vya maji na kuendelea kufanya kwa kijificha katika kichaka ya kuwa elimu hayatolewa.
Kwa upande Afisa Maendeleo wa Bodi hiyo Hawu Sarwat amesema kuwa wamefanya ukaguzi katika shamba hilo na kuweza kuona makosa yanajirudia.
Amesema kuwa kwa hali ya sasa ukaguzi utakuwa endelevu na atakayekutwa hatakuwa salama kwao na mashine au mitambo yao.