Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema anashangazwa na Magaidi wanaojitoa muhanga kwa kujilipua wakidai watakwenda Mbinguni moja kwa moja huku akihoji kama hilo lina ukweli kwanini Viongozi wao hawajilipui bali wanawatumia Vijana wenye umri mdogo.
"Kama kujilipua na bomu kunamfanya Mtu aende Mbinguni kwanini Viongozi wa haya makundi ya Kigaidi wasioneshe mfano kwa kujilipua, Watu wa kwanza kujilipua wanapaswa kuwa hawa Viongozi lakini wao wanakaa nyumanyuma na kuwatuma Watoto wadogo wajilipue"
Kama Umependa Habari Hizi Download APP ya UDAKU SPECIAL Kwenye Simu Yako Kwa Kubonyeza >>HAPA
"Niwape pole waliopoteza Ndugu zao kwenye matukio ya milipuko miwili ya hivi karibuni lakini nawahakikishia tutamaliza Ugaidi Uganda, tuna Intelejensia nzuri sana"