Muswada Bima ya Afya kwa Wote Wakamilika





Wizara ya Afya imesema tayari imekamilisha muswada wa Bima ya Afya kwa Wote (UHC) na sasa upo tayari kufikishwa katika muhimili wa Bunge.


Hayo yamesemwa leo Jumatano, Novemba 17, 2021 na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima wakati wa mkutano wa mwaka wa kisayansi wa huduma za afya ya uzazi, mtoto, vijana na lishe wenye lengo la kuongeza kasi ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi, watoto wachanga, watoto chini ya miaka mitano na vijana.



Dk Gwajima amemweleza Waziri Mkuu kwamba maelekezo ambayo aliyatoa kuhusu muswada huo yamekamilika na kwamba sasa wizara inasubiri maagizo kutoka kwake.



“Tunatambua kwamba muswada wa bima ya afya kwa wote ni muhimu katika kutatua changamoto za tiba nchini na nikwambie



tu kwamba tumeshatekeleza maagizo uliyotupatia tayari tunasubiri mwongozo wako,” amesema Dk Gwajima.



Awali akitoa neno kwa niaba ya asasi za kuraia, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation, Dk Ellen Mkondya-Senkoro amesema bima ya afya kwa wote ni suala mtambuka ambalo likitekelezwa itasaidia kurahisisha matibabu nchini.



“Ni asilimia 14 pekee ya Watanzania ndiyo waliopo kwenye mfumo wa bima ya afya, suala hili ni mtambuka hivyo Serikali isisite kutushirikisha asasi za kiraia katika muswada utakaopelekwa bungeni ili nasi tuweze kutoa maoni yetu,” amesema Dk Senkoro.



Awali Wizara hiyo ilisema muswada huo ungesomwa bungeni Novemba mwaka huu, lakini kutokana na kukosekana kwake, Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema suala hilo linafaa kushughulikiwa haraka.



“Bima inagusa Watanzania wengi hususan wa kipato cha chini huu ni muda mwafaka kwa muswada huu kufikishwa ili itungwe sheria.



“Ni muhimu Serikali ikasema kama kuna mkwamo mahali ili Bunge lisaidie,” alisema Spika Ndugai.



Katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali ilitenga bajeti ya Sh149 bilioni kwa ajili ya utekelezaji wa mpango wa bima ya afy

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad