Hivi itakuaje pale ambapo utakutana na mwalimu uliyempenda ambaye amekufundisha miaka 20 iliyopita !!!?
Sasa Furaha hii imefanya Mwimbaji Adele Aangue kilio baada ya kumuona mwalimu wake kipenzi aliyemfundisha Akiwa shule zaidi ya miaka 20 iliyopita .
Adele alirejea hivi karibuni katika mji aliozaliwa na kutumbuiza katika ukumbi wa London Palladium katika show kubwa iliyokuwa live kwenye kituo cha ITV cha nchini Uingereza mbele ya Hadhira ikiongozwa na mastar wakiwemo Daniel Kaluuya, Emma Watson na Hannah Waddingham.
Sasa wakati wa Onyesho hilo Adele aliulizwa na Mwigizaji Emma Thompson kama ana mtu yeyote ambaye alimtia moyo alipokuwa mdogo .
Adele ambaye amezaliwa Tottenahm Uingereza alijibu kuwa kuna mwalimu wake kutoka Chestnut Grove shule iliyopo kusini mwa London anaitwa McDonald alimfundisha Fasihi ya kingereza anasema alimjali sana sio yeye tu bali pia wanafunzi wengine kwamba alibadilisha maisha yao .
Baada ya kuzungumza hivyo mara ghafla akatokea Mwalimu huyo aliyekuwepo kwenye Audience ya watu waliokuwa wakitazama show hiyo na alipokuja kwa stage adele alimwaga machozi ya furaha na Kumkubatia .
Adele aliweka wazi kuwa hakumuona mwalimu wake tangu akiwa na miaka 12 na hapo hapo ilibidi ampatie namba yake ya Simu wakataniana pale ikawa Furaha sana kwao .
Adele ameachia album yake ya 4 Mwezi huu November iitwayo "30 "ambayo ilipata Streams million 60.7 siku ya kwanza kuachiwa kwake na kuifanya kuweka rekodi kubwa katika Career yake muziki .