Mwanamuziki Aboubakar Shaban Katwila maarufu #QChief amefunguka namna ndugu upande wa Baba yake walivyokuwa wakimtesa hadi kufikia hatua ya kutaka kumtoa kafara, kumuua lakini kwa uwezo wa Mungu imeshindikana.
#QChief ambaye anafahamika kwa uwezo wake mkubwa na mzuri wa kuimba. Akiwa pia na mchango mkubwa kwenye gemu la Bongo Fleva ametumia ukurasa wake wa instagram kuyaweka wazi hayo, pia akimshukuru Mungu kwamba ibada anazozifanya kwasasa ndizo zilizomuokoa kutoka kwenye matatizo na nduguze.
Aidha, ametumia ukurasa wake huo pia kuwaonya ndugu hao ambao pia wamemfollow, endapo wakiendelea kufanya waliyokuwa wanayafanya basi makubwa mengine yatawakuta.
Soma jumbe zote za #QChief