Mwanamuziki ambae alikua akitajwa kama msani atakae tambulishwa katika record label ya WcB Wasafi @thehanstone ameonekana kuvunjwa moyo na hali ya muziki wa tanzania unavyokwenda kwasasa.
Kupitia insta story yake #hanstone ameonesha hali hiyo baada kushere ujumbe wenye emoji ya kopa lililovunjika pamoja na bendera ya tanzania na kuandika neno music ,ujumbe ambao moja kwa moja unatafsirika kama kuvunjwa moyo na hali ya muziki nchini, licha ya yeye mwenyewe kutoweka wazi tafsiri halisi ya alicho maanisha kwenye post hiyo.
“💔🇹🇿music!!! ”
Tayari mwanamuziki huyo ambae alitamba kwa verse zake kali kwenye nyimbo ya 'iokote' ya maua sama na 'chibonge' ya producer abbah, ameachia EP' yake aliyoiita Amaizing yenye jumla ya nyimbo 7.
✍🏾@keviiiy.iam