Mwenyekiti Simba Afunguka Chama Kurudi

 





MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah Muhene “Try Again” leo Novemba 21, 2021 akiongea na wanachama wa klabu hiyo katika Mkutano Mkuu wa Simba mwaka 2021 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere amesema Simba inakwenda kutetea tena ubingwa wake.

 

Pia amesema kuwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ amesema kuwa mzigo wa usajili upo na kuongezea kuwa awe Chama na wengine watawasajili.

“Nataka niwambie Simba inakwenda kutetea tena ubingwa wake, hilo hakuna shaka kabisa. Nia tunayo, uwezo tunao, nguvu tunayo, pesa tunazo. Nini cha kutuzuia?”.

“Kwa kutambua mchango wake mkubwa na makubwa aliyotufanyia kwenye klabu hii, kwa mapenzi makubwa kwa klabu hii katika kikao cha bodi kilichokaa hivi karibuni Bodi imeamua kumpa Urais wa heshima Ndugu Mohammed Dewji “

 

“Kwa wafanyakazi wa Simba kuanzia wachezaji hadi menejimenti, ndani ya Simba hakuna mkubwa kuliko Simba. Wanachama mtuelewe tunapofanya maamuzi magumu, hatuwezi kukaa na mtu anayetusaliti.”- Mwenyekiti wa Bodi, Salim Abdallah Muhene “

 

“Hizi kelelekelele zisiwanyime usingizi. Tutawapita kama wamesimama. Watashangaa. Nasema haya sababu tunayo jeuri. Simba imewekeza kwenye mpira, Simba haijawekeza kwenye kejeli, fitna na vijembe, hayo hayana tija kwetu tumeshapita huko, sisi WE ARE NEXT LEVEL. Wanasimba mna kila sababu ya kutembea kifua mbele. Watake wasitake mpira utachezwa.”

 

“Nawahakikishia Disemba 11 tutawapiga. Mbinu zote tunazijua. Tunachowaomba mashabiki ni umoja na ushirikiano.” amesema Mwenyekiti wa Bodi, Salim Abdallah Muhene “Try Again”.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad