Kwenye kijiji kimoja katika milima huko Scotland, Tonks Brown anasema anajivunia kuwa mchawi.
Tonks Brown
Kwake sherehe za Halloween hazihusu tu mavazi, maboga au matibabu
“Ni zaidi ya hayo: Ni sehemu kubwa ya maisha yangu, ni dini yangu na imani yangu, anasema Tonks mwneye umri wa miaka 36.
Mwaka mpya wa pagani ni Novemba mosi na Tonks anasema tarehe hiyo inaashiria mwanzo mpya.Una escoba de bruja y un gato negro llamado Cairn
Tonksana chumba cha uchawi na paka mweusi anayeitwa Cairn.
Alibadilika na kuwa mpagani akiwa umri wa miaka 12 akiishi eneo lijulikanalo kama Isle of Mull kaskazini magharibi mwa Scotland.
“Nilionewa nikiwa shule ya sekondari kwa kuwa tofauti,” anasema.
Wanililazimisha kuhudhurua kanisa la We Free Church nikiwa shuleni, kulikuwa na ibada na maombi kila wakati.”
“Nakumbuka nikikemewa kwa kujichora wakati nilitakiwa kuomba.”
Asili, ndio “kanisa lake”
Tonks anasema ni nje ya kanisa ambapo anahisi hayuko peke yake na kuwa wanyama na pia ni viumbe wenye akili.
“Nilimuondoa konokono kutoka barabarani ili asikanyagwe,” anasema.
“Ni wakati huu ndio nilikuja kugundua kuwa asili ndio kanisa langu badala ya jengo kubwa.”
Anadai aligundua kuwa upagani ulikuwa mzuri na wa maana kwake.”
“Kila kitu katika asili kina kusudi lake na ni vizuri kuwa na uelewa kama huo,” anasema.Pia akaanza kusoma kuhusu hukumu za wachawi za nyakati zilizopita.
“Kwa bahati mbaya watu wengi wachawi huwa ni wanawake, wanawake wenye ujuzi, wakunga, madaktari wa kienyeji,” anasemaTonks
Unafanya nini katika maisha yako ya kila siku?
Tonks hufanya kazi kwenye huduma za dharura katika jamii yake.Tonks Brown
Huendesha gari dakika 10 kila siku ndani ya kijiji ambapo ana ofisi.
Anasema amejifunza kutohubiri kuhusu upagani lakini huwa anawatetea wachawi katika maisha yake ya kila siku.
“Nikiskia mtu akifanya mzaha kuhusu mchawi huwa ninaingilia kati na kusema mimi ni mchawi,” anasema.
Mwanamke ambaye alikuwa muelekezi wa safari huko Edinburgh anasema alifanya kazi na serikali za miji, polisi na magari ya kubeba wagonjwa lakini upagani wake sio tatizo.
Uchawi wake
Sherehe zake zinahusu kufanya upagani na uchawi.
Amekuwa akikuza mimea kadhaa kwa mwaka mzima kwa sherehe zinazohitimisha msimu wa mavuno au kuanza kwa msimu wa baridi.Tonks Brown
Akichoma mitishamba
Hukausha mimea kwa moto ili iweze kuchomwa kwa njia bora wakati anaitumia.
Anachoma mimea hiyo kujisafisha na nyumba yake kwa kutumia moshi. Na ina chumvi na madini ya chuma kuwafukuza mizimu.
Pia amekuwa akiiwekea mishumaa mafuta tofauti na mimea na pia kuichonga ili kutumia kwenye siku kuu.
Mchawi mweupe
Wachawi weupe kama Tonks, hawafanyi uchawi kwa nia mbaya.
Wao hutumia matambiko kutafuta mimea, Tonks anasema kawaida yeye huwa peke yake wakati anafanya matambiko yake.Calabazas de fieltro en la casa de Tonks Brown
Katika uchawi wake hutumia maboga na mizizi kuwatisha mizimu
“Ninawafahamu wachawi wengine wengi, tuko kila mahali, idara ya polisi, kwenye maduka ya kijijini, lakini mimi sishiriki nao uchawi, lazma uwe na ujasiri,” anasema.
Wachawi waupe husoma kitabu cha giza.
“Siku hizi mimi nasimama nje na kuwaambia watu kuwa mimi ni mchawi na asilimia 99 hujibu vile wangeweza iwapo ningesema mimi ni Mkiristo au Muislamu,” anasema.
Nijivunia kuwa mchawi na Halloween ndiyo sherehe bora zaidi.
Kwa zaidi ya miaka 13 ya ndoa sikuweza kuzaa, naendelea kuharibika hata nikipata mimba, madaktari wote hawakuweza kunisaidia, hadi dada yangu akanielekeza kwa Dr DAWN, ambaye alinisaidia nikapata ujauzito na sasa hivi kuwa na mtoto mzuri wa kike,
ReplyDeleteAnasaidia pia marafiki zangu wengi niliowaelekeza, Dr DAWN ni baraka kwa kila mtu anayewasiliana naye,
*Kama unataka kupata mimba.
*Ukitaka kuacha kuharibika kwa mimba.
*Ukitaka kumrudisha mpenzi wako.
*Kama unataka mume/mkeo arudishwe.
*Kama unataka kurejesha mali yako iliyoibiwa au Pesa.
*Ukitaka kutibu aina yoyote ya ugonjwa,
Wasiliana naye kwa WhatsApp: +2349046229159