Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye, ameitaka Serikali kufanya ukaguzi kuhusu Mikopo iliyokopwa na Serikali katika kipindi cha awamu ya tano ili kujua Uhalisia wa Matumizi ya mikopo na Deni la Taifa iwapo ni himilivu.
Nape ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya 5 ilikopa mikopo mingi huku asilimia 40 ya mikopo hiyo ikiwa ni ya kibiashara hivyo kuwa na riba kubwa.
Ameongeza kwa kutaka uchunguzi ufanyike jjuu ya mikopo hiyo na ilinganishwe na thamani ya miradi ambayo mikopo hiyo ilifanya.
Ameipongeza Serikali ya awamu ya 5 kwa kuweka wazi mkopo wa 1.3 trilioni iliyokopa kitu ambacho hakikuwepo kipindi kilichopita na kutaka uwazi huu uigwe.