SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema ipo haja ya kufungua Mjadala wa Elimu, na ndiyo maana Wabunge wamekuwa wakisema washirikishwe.
Akiwa Bungeni Dodoma amemwambia Waziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalichako, “Sisi tunataka Elimu ya Tanzania tuitazame. Hayo sijui ipo Wizara gani, sisi kama Wananchi haituhusu, tunataka tuseme tunataka nini kwenye Elimu…”
Ameongeza, “Tena Elimu ya Chuo Kikuu ndiyo watu wanalalamikia kuliko hata ya chini. Mliangalie vizuri ndani ya Serikali, namna gani ya kushirikishana…”