Nyota wa YouTube nchini Rwanda, Dieudonné Niyonsenga amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela kwa kuikosoa serikali.
Niyonsenga anayejulikana kama Cyuma au “Iron”, alipatikana na hatia ya kughushi, uigaji na kuwadhalilisha maafisa wa serikali ambapo video zake zilionekana akiwashutumu askari kwa unyanyasaji mkubwa dhidi ya watu wa hali ya chini wakati wa marufuku ya kutoka nje katika kipindi cha janga la Corona.
Licha ya kukana mashtaka hayo, lakini mahakama imamlima nyundo ya miaka saba jela huku mwenyewe akisema hajaridhika na maamuzi hayo ya mahakama hivyo atakata rufaa.
Mtu mwingine maarufu wa YouTube hivi karibuni alihukumiwa kifungo cha miaka 15 kwa kuchochea vurugu. Mamlaka ya Rwanda mara kwa mara inashutumiwa kwa kukandamiza upinzani na kuwafunga jela wale wanaoikosoa serikali.