Picha za CCTV zaonesha mumewe mwanariadha Agnes alikuwa aneo la mauaji





Mwanariadha Agnes Tirop alipatikana amefariki dunia mnamo Jumatano, Oktoba 13, ndani ya chumba chake cha kulala huko Iten
Ripoti ya upasuaji wa maiti iliomesha kwamba Tirop alipigwa na kifaa butu, akakatwa kichwa, pamoja na kudungwa kisu mara kadhaa shingoni
DCIO wa kaunti ndogo ya Keiyo Kaskazini Andolo Munga alisema kanda za CCTV zilionesha kuwa Tirop aliuawa alasiri ya Jumanne, Oktoba 12, 2021
Kanda za picha za CCTV zimeonesha kuwa mume wa marehemu mwanariadha Agnes Tirop, Ibrahim Rotich ni mshukiwa mkuu wa mauaji ya nyota huyo.

Agnes Tirop: Picha za CCTV Zammulika Mumewe mwanariadha Katika Eneo la Mauaji
Picha za CCTV zilionesha kuwa mumewe Agnes Tirop alikuwepo katika eneo la maujai ya mwanarisha huyo. Picha: Athletic Kenya.
Picha hizo zilionyesha kuwa mshukiwa alikuwa katika eneo la uhalifu nyumbani kwake Iten siku ambayo Tirop aliuawa kikatili.

Kulingana na DCIO Andolo Munga wa kaunti ndogo ya Keiyo Kaskazini, picha za CCTV zilifichua kuwa mwanariadha huyo aliuawa alasiri ya Jumanne, Oktoba 12, 2021.

"Picha za CCTV zinajieleza wazi baada ya uchambuzi wa kitaalamu. Ina ushahidi wote wa tukio na kitendo halisi. Tunaamini hapa tuna kesi na sasa tutaendelea na mashtaka,” alisema mpelelezi huyo.


 
Raila Asisimka kwa Kupokelewa Vyema kwa Shangwe na "Wasee wa Kanairo"
Katika ripoti ya Daily Nation, Munga alisema kuwa picha hizo zilionyesha kwa usahihi kile kilichotokea na jinsi kilifanyika hadi pale Tirop alipofariki dunia.

Hapo awali, TUKO.co.ke iliripoti kuwa Rotich alikuwa amezuiliwa kwa siku 20 ili kuruhusu polisi kukamilisha uchunguzi kuhusu madai yake ya kuhusika katika mauaji ya mwanariadha huyo.

Rotich alifikishwa mbele ya Hakimu Charles Kutwa, ambapo upande wa mashtaka ulitaka muda zaidi wa kumzuilia.


Mahakama iliamuru mshtakiwa azuiliwe katika Kituo cha Polisi cha Railways mjini Eldoret.

Pia atafanyiwa uchunguzi wa kiakili katika Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Eldoret.

Tirop alipatikana akiwa amefariki dunia asubuhi ya Jumatano, Oktoba 13, akiwa na majeraha ya kisu shingoni na tumboni katika nyumba yake huko Iten, Kaunti ya Elgeyo Marakwet.

Mumewe, ambaye alitoweka baada ya kisa hicho, alikamatwa usiku wa Alhamisi, Oktoba 14, Changamwe, Mombasa.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad