Pingamizi Jingine la Mbowe ‘Lauma Chuma’





Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Joachim Tiganga ametoa uamuzi kuhusu Shahidi aliyejitambulisha kama askari H4323 DC Msemwa wa kituo cha Polisi Oyster Bay ambaye alikutwa na Simu, Diary na Kalamu wakati akitoa ushahidi dhidi ya Freeman Mbowe na wenzake watatu.

 

Jeremiah Mtobesya ni miongoni mwa Mawakili wa upande wa Utetezi ambaye amesema vitu alivyokutwa navyo Shahidi vilipelekwa mbele ya Mahakama ingawa wakati wa kufunga siku hiyo Mahakama ilielekeza kwamba ni Busara Shahidi arudishiwe Simu yake na suala likabakia kuwa ni Diary.

 

Mahakama imetupilia mbali pingamizi la mawakili wa utetezi katika kesi ya Freeman Mbowe na wenzake watatu. Mahakama imekubali hoja za upande wa mashtaka na kukubali barua iliyotolewa na Naibu Msajili wa Mahakama itolewe kama kielezo na shahidi namba mbili katika kesi ndogo.

 

Jaji Joachim Tiganga amesema Mahakama inashindwa kuona Shahidi huyo siyo mkweli, upande wa utetezi wanayo nafasi wakati wa dodoso, wanaweza kumpima Shahidi huyo kama mkweli au siyo mkweli, kielelezo kinatakiwa kisomwe lakini ku’ refer content ili aweze kutambua nyaraka hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad