Pingamizi la Mbowe Lagonga Mwamba



JAJI Joachim Tiganga ametupilia mbali pingamizi lililowekwa na upande wa utetezi katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

 

Katika pingamizi hilo, mawakili wa utetezi walipinga mahakama hiyo kuipokea hati ya ukamataji mali za washtakiwa wawili katika kesi hiyo.

 

Huu hapa ni uamuzi kama ulivyotolewa na Jaji Joachim Tiganga;

Jaji Tiganga ndio anaingia katika ukumbi wa mahakama.

Upande wa mashtaka wameanza kuitambulisha safu ya jopo la mawakili tisa wakiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando

 

Jaji Tiganga anaanza kusoma uamuzi wa pingamizi la upande wa utetezi kuhusu kupokewa hati ya ukamataji mali kutoka kwa washtakiwa walizokutwa nazo wakati wakiwapekua baada ya kuwatia mbaroni mjini Moshi.

Jaji Tiganga anaanza kurejea chanzo na hoja za pingamizi.

Sasa Jaji Tiganga anarejea majibu ya mawakili wa Serikali dhidi ya pingamizi hilo.

 

Kwa sasa Jaji Tiganga anarejea tena hoja na majibu ya upande wa utetezi kufafanua hoja zilizoibuliwa na upande wa mashtaka.

Baada ya kurejea hoja za pande zote, sasa Jaji Tiganga anaanza kufanya uchambuzi wake kabla ya kufikia hitimisho la kukubakiana na pingamizi au kulitupilia mbali.

 

Kama mahakama itakubaliana na pingamizi basi itaikataa hati hiyo ya ukamataji mali na haitapokewa kama kielelezo cha upande wa mashtaka na kama mahakama italikataa pingamizi itaipokea na kuwa kielelezo cha ushahidi wa mashtaka.

 

JAJI: Pingamizi la utetezi liko wazi na ni la moja kwa moja

Wakati nafanya maamuzi haya nimebaini kuwa mawakili wa pande zote wamekwenda mbali zaidi na kuleta hoja nje ya hoja ya msingi, ambazo pia zimeisaidia mahakama lakini uamuzi wangu utajikita kwenye suala la msingi yaani upokeaji wa kielelezo ingawa haina maana ya kupuuza hoja za ziada zilizoketwa na mashahidi

 

Hoja ya pingamizi inaonyesha sheria ambayo fomu hiyo imeandaliwa kwayo imekosewa hivyo nineona niende moja kwa moja kwenye fomu hiyo kuona ilivyoandikwa.

Sasa Jaji Tigana anaisoma fomu hiyo ya hati ya ukamataji mali kama ilivyoandikwa

Neno lililoleta ubishi ni sheria iliyorekebishwa ambalo nimelipigia mstari maana ndilo lililoleta mvutano

 

Mawakili wa pande zote hadi wanamaliza hoja zao hawakuweza kutoa maana halisuni ya neno iliyorekebishwa hivyo mahakama imeona ni vizuri ikatafuta zaidi maana ya hilo neno.

Nimepata Kamusi ya Kiswahili ya TUKI lakini pia sijapata maana ya moja kwa moja ya neno iliyorekebishwa ila nimepata kitenzi rekebisha kwa Kiingereza adjust or amend.

 

Kwa hiyo kilichoko mbele ya mahakama tafsiri yake si mapitio (Revised)

Japo fomu hiyo imenukuu kimakosa kuwa sheria hiyo imetajwa kimakosa kuwa imerekebishwa mwaka 2108, matokeo yake nyaraka hiyo inakuwa na mapungufu kisheria ambayo yanaweza kuifanya isiwe na nguvu

Hata hivyo kanuni hiyo ya kutaja vibaya sheria inafanya nyaraka hiyo ikose nguvu haitumiki katika mazingira yote bali hutegemea mazingira ya shauri husika.

 

Kuna maamuzi mbalimbali kuwa nyaraka ambayo lazima itaje sawasawa ni ile inayoleta maombi kuomba mahakama kufanya au kutoa mamuzi fulani na si kwa nyaraka kama hii inayohusu ukamataji mali.

Kuna maamuzi mbalimbali ya Mahakama ya Rufani kuwa katika mazingira kama ya nyaraka hii malengo yake yanatofautiana na malengo ya nyaraka ya kuiomba mahakama kuyeteleza majukumu yake.

 

Mahakama ya Rufani imeweka kanuni mpya kuwa malalamiko tu kuwa nyaraka hiyo ina mapungufu hakuifanyi nyaraka hiyo kufa bali ni lazima mlalamikaji aeleze kukosea kutaja sheria husika kunamuathiri vipi.

Mahakama Kuu nayo kwa sasa imekuwa na mtizamo huo kufuata msimamo wa Mahakama ya Rufani kwamba kukosea kutaja kifungu cha sheria kunaifanya hati husika kufa.

 

Mahakama hii inajiuluuza kama mlalamikaji anatakiwa aonyeshe kuwa kutajwa kimakosa kwa Sheria hiyo kumemuathiri basi inaweza kutibika katika hali hiyo mahakama inaona kuwa katika mazingira ya shauri hili utetezi haujaonesha kukosea kutaja sheria hiyo kunewaathiri vipi na kwa kuwa wanayo nafasi ya kumuuliza shahidi maswali basi mahakama inatupilia mbali pingamizi hili na inapokea kielelezo hiki.

Sasa Jaji Tiganga anaelekeza shahidi aisome nyaraka hiyo kwa sauti na shahidi anaanza kuisoma nyaraka hiyo.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad